ad

ad

Kaseja: Tukishinda mechi moja tu, Kagera inarudi kwenye mstari




Mlinda mlango na nahodha wa Kagera Sugar, Juma Kaseja amesema, wakishinda mechi moja moja tu, timu yao inakaa vizuri.

Kaseja ambaye kikosi chake kinashika mkia na pointi moja licha ya kucheza michezo minne, imetoa sare moja na kufungwa mitatu ikiwamo kipigo cha 1-0 leo Jumapili kutoka kwa Stand United .
"Timu haitengenezi nafasi ni kazi ya benchi la ufundi. 


Wao ndiyo wanaona ni sehemu ipi ina mapungufu na kwa namna gani watafanya marekebisho ili mambo yaende sawa," alisema Kaseja baba wa watoto pacha aliowapata mwaka jana.

"Lakini, lichi bado mbichi, ndiyo kwanza mechi ya nne, tuna nafasi kubwa mbele, tukifanya vizuri na kushinda mchezo mmoja tu, Kagera inakaa sawa."
Kagera ambayo msimu uliopita, ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu, sasa mechi ya nne inashika mkia.

No comments

Powered by Blogger.