A-Z Ya Mshindi wa Shinda Nyumba Alivyopatikana (Video)
Diwani ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi. Mheshimiwa diwani akiwa kwenye rundo la kuponi Mheshimiwa diwani akichanganya kuponi. Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi. Mheshimiwa diwani akiwa ameiinua kuponi juu Diwani Lema akisoma jina la mshindi wa nyumba, aliyemshikia kipaza sauti ni MC Chaku. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba. Meneja Mrisho akipeana mikono na Diwani Lema Diwani Lema akizungumza na watu waliofika kushuhudia droo hiyo Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set. Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set. Mhariri wa Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) akiwa na mhariri mwenzake, Sifael Paul anayesimamia Gazeti la Ijumaa Wikienda. Abdallah Hemed (kushoto), afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, akiandika jambo huku akifuatilia droo hiyo, pembeni yake ni Meneja Mrisho
Hatimaye Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba iliyokuwa ikiendeshwa kwa zaidi ya miezi 6 na Kampuni ya Global Publishers ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wasomaji wake, imefikia mwisho ambapo mshindi kutoka Dodoma amepatikana. Katika droo ya fainali hiyo, ambayo imefanyika kweNye Viwanja vya Las Vegas, Mabibo jijini Dar huku mgeni rasmi akiwa Diwani wa Kata ya Mabibo, Kassim Lema, mshindi aliyejishindia nyumba hiyo iliyopo Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar, ni George Majaba mkazi wa Mkoa wa Dodoma. Akizungumza na Gazeti hili, mapema baada ya kumaliza shughuli ya kumtangaza mshindi wa nyumba hiyo, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho aliwashukuru wasomaji wa Magazeti ya Global kwa kuwa waaminifu katika kipindi chote ambacho wameshiriki kimamilifu kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mshindi. Mbali na mshindi huyo wa nyumba, pia kulikuwa na washindi wengine walioibuka na zawadi za dinner set, ambao ni Kahabi Suleiman wa Vingunguti, Dar, Melania Swai wa Mbezi, Dar na Philemon Faustine wa Dar.

Post a Comment