ad

ad

WIMBO WA ALIKIBA WAMKUNA CHRISTINA SHUSHO AMUITA KIBA KANISANI

IKIWA ni siku mbili tu tangu, mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘King Kiba’, aachie kibao chake cha Seduce Me, ngoma hiyo imeendelea kukuna mioyo ya mashabiki wake,

akiwemo muimbaji wa Injili nchini Christina Shusho, ambaye ameweka wazi mapenzi yake juu ya wimbo huyo kwa kuposti katika ukurasa wake wa Instagram.

Akiandika kwenye ukurasa wake huo, Shisho alisema: “Leo unaweza kukuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha Seduce Me, Eeh jamani Kiba we noma, wimbo ni mzuri sana kitaaluma kama anavyopenda kusema bosi Ruge.

“Hauna picha za aibu, naweza kuuangalia nikiwa na familia, labda sijui maana ya Seduce Me. Timu Kigoma Wamanyema oyeeeee.

“Cha mwisho Ali Kiba basi siku nyingine tutembelee kanisani ukiwa mfalme huchagui dini wote wako” ameandika Christina Shusho.

Wimbo huo umeweka rekodi ya kutazamwa zaidi ya mara milioni 1 ndani ya saa 38 tangu ilipoweka kwenye mtandao wa You Tube.

No comments

Powered by Blogger.