Taarifa Rasmi ya Jeshi la Polisi Kuhusu Wahalifu 13 Waliouawa Kibiti
Tarehe
09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya
kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda
kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya
uhalifu.
Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu @Mtawa
6. Rajabu Thomas @Roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
|
KIELELEZO
|
UTAMBUZI
|
SILAHA, RISASI NA MABOMU
|
||
1.
|
SMG = 5
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
2.
|
Anti Riot Gun 38mm = 2
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
3.
|
SAR = 1
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
|
4.
|
MAGAZINI = 2
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
5.
|
Risasi za SMG 158
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
6.
|
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
|
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
|
7.
|
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
|
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
|
VIELELEZO VINGINE
|
||
8.
|
Pikipiki = 2
|
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
|
9.
|
Vitenge na Nguo mbalimbali
|
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
|
10.
|
Begi = 1
|
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe
|
Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo
vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya
watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu
maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba
eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa
Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha
nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi
wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani,
hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli
zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa
waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu
kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo
ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao
umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya
Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu
Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho
kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata
taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu
kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa
ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao
wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa
wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.
Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la
Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na
anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya
Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi
maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba
taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa
kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara
moja.
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu
watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili
waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula
Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo
hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama
imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea
kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia,
kubambana na kutanzua uhalifu nchini.
Imetolewa na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
Post a Comment