Thea: Fimbo za Dingi Zimekuwa Dira Maishani Mwangu!
Salome Urassa ‘Thea’.
alimuwekea misingi ya nidhamu na alipokengeuka alidhibitiwa kwa fimbo hata alipokuwa mama.
Katika kubadilishana mawazo juu ya maisha na mwandishi wetu hivi karibuni, Thea ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike watulivu, alisema kuwa, nyumbani kwao kuna kanuni na tamaduni za kikoloni hivyo hakuna mtoto aliyekua hana maadili na misingi bora ya maisha.
“Weee! Baba yangu alikuwa kiboko, mimi mwenyewe nilikuwa napigwa fimbo na ukubwa wangu huu, nakumbuka kuna siku nilikwenda kumtembelea rafiki yangu, tena si miaka mingi sana, lakini nililala huko bila ruhusa ya wazazi, niliporudi kesho yake, nilishushiwa kichapo cha mbwa koko, kwa hiyo niko hivi nilivyo kwa sababu ya malezi bora ya baba yangu hususan fimbo zake,” alisema Thea.
Post a Comment