Serikali yampa Gwajima masharti ya kuingiza ndege yake nchini
Siku
moja baada ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu
Joesphat Gwajima kusema kuwa ataileta Tanzania ndege yake binafsi,
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekana kuwa na taarifa
kuhusu ujio wa ndege hiyo.
Ofisa Habari wa TCAA, Ali Changwila alisema kuwa hawana taarifa kwamba Askofu Gwajima ana mpango wa kuingiza ndege yake nchini.
Juzi
Askofu Gwajima alithibitisha kununua ndege hiyo aina ya Gulfstream
N60983 yenye thamani ya Tsh 2.64 kwa ajili ya kuendeleza ufalme wa
Mungu.
Askofu
Gwajima aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amesimama
mbele ya ndege hiyo ambapo alisema karibuni itawasili Tanzania kwa ajili
ya shughuli zake za injili.
TCAA
imesema kuwa Mtanzania yeyote anayenunua ndege nje ya nchi na kutaka
kuiingiza nchini anatakiwa kwanza kuitaarifu mamlaka hiyo ili iweze kuwa
na taarifa kamili. Aidha, alisema kabla ndege hiyo haijaingizwa nchini
ni lazima wataalamu wa TCAA wajiridhishe kuwa wanaifamahu na ifanyiwe
ukaguzi.
TCAA
imesema ndege hukaguliwa kabla haijaingizwa nchini ili kujirisha kuwa
inakidhi vigezo vya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).
Mbali
na vigezo hivyo, wanakagua pia kama ina vyeti vya usajili, historia
yake, imekwisha muda wake? imeshakatazwa kusafiri? Ukaguzi wote huo ni
kuepuka kutumia ndege ambayo muda wake wa matumizi umepita, kwani baadhi
ya watu huuza ndege ambazo muda wake wa kutumia umekwisha.
Baada
ya wataalamu kujiridhisha na vyote hivyo, ndege hiyo itatakiwa kujaza
fomu ya TCAA ili iweze kufuata sheria za nchi ambapo itaelezwa itarushwa
na rubani gani na itatumia viwanja gani.
Post a Comment