NUH MZIWANDA: Kuoa Tena Namuachia Mungu
MWANAMUZIKI Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambaye hivi karibuni mkewe, Nawal alifunga ndoa na mwanaume mwingine amefunguka kuwa, kwake kuoa tena anamuachia Mungu.
Akibonga na Mikito Nusunusu, Nuh alisema baada ya mkewe kuondoka na kuamua kuolewa bila kumpa talaka suala la kuoa au kutokuoa anamuachia Mungu na kwamba hajaathirika chochote kuhusiana na mkewe kumuacha ila anachofanya kwa sasa ni kuongeza bidii katika kazi.
Nuh Mziwanda.
“Namwachia Mungu ndiye anayejua kama
nitaoa au sitaoa tena, ikitokea sawa na isipotokea inakuwa sawa tu kwa
sasa moyo wangu una amani tele na nimerudi kwenye dini yangu ya
Kikristo, kuhusu mwanangu ataendelea kuwa wangu na mahitaji yote muhimu
natoa kama baba,” alisema Nuh.


Post a Comment