NIMETOKA KIMAPENZI NA SOUDY WA ‘SHILAWADU’ KWA MIAKA MIWILI – RUBY
Msanii wa muziki Ruby amefunguka kwa kudai kuwa alitoka kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds FM, Soudy Brown kwa miaka miwili lakini baadaye alikuja kuachana naye baada ya kuona hana msimamo.
Ruby amedai Soudy Brown ndiye mwanaume pekee aliyetoka naye kimapenzi kutoka kwenye industry ya muziki.
“Nikisema nitoke na mastaa wenzangu sio kwamba hawanisumbui wananisumbua sana lakini nawajua tayari the way walivyo,” Ruby aliuambia mtandao wa Spin Tanzania. “Lakini vitu vingi ambavyo naona wanafanyiwa wasanii wenzangu na mimi kweli nikawe na msanii? Hapana siwasemi kwa sifa mbaya wasanii lakini mimi siwezi kuisha nao kutokana na tabia zao kwa sababu mimi ni mwepesi sana kuumia,”
Aliongeza,”Mimi mwanaume ambaye nimetoka naye kwenye mapenzi na yupo kwenye industry yetu only ni Soudy Brown, na nimeishi naye kwa mwaka mmoja na miezi sita,”
Pia muimbaji huyo wa ‘Na Yule’ alikanusha tetesi kwamba alibeba mimba na kuitoa ya mtangazaji huyo ambaye anaendesha kipindi cha Shilawadu cha Clouds FM.
Post a Comment