Mwakyembe: Najua presha inapanda na kushuka Uchaguzi Mkuu TFF
WAZIRI
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr, Harrison Mwakyembe amesema anaamini
presha zimekuwa za kupanda na kushuka kwa wagombea na wajumbe wa Uchaguzi Mkuu
wa Shirikisho la Soka Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kupata viongozi
bora.
Uchaguzi Mkuu wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St
Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na
wajumbe wa kamati ya utendaji.
Uchaguzi huo
unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli
unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi
cha miaka minne.
Mwakyembe
anasema: “Ninajua presha imekuwa ya kupanda na kushuka siyo tu kwa wagombea
bali na wajumbe na ninajua ni kwa nia nzuri tu ya kupata viongozi bora na
adhimu kwa maendeleo ya soka nchini Tanzania.
“Viongozi
bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo
usiotetereka kwa vishawishi vya mpito.
“Serikali
inaamini tuna wajumbe makini, wasioyumbishwa kwa vishawishi vya muda, mpito wanaoongozwa
na dhamira njema na uzalendo wa hali ya juu ambao watatuibulia viongozi bora wa
TFF wenye ari na moyo.”
Post a Comment