Mtatiro: Bora CCM kuliko kufanyakazi na Prof. Lipumba
Amesema
kuwa hilo ni jambo ambalo halitawezekana tena kwao kukubali yaishe,
hivyo hawawezi kukaa meza moja na Profesa Ibrahim Lipumba kwani alishaga
jiuzuru katika harakati za Kampeni za uchaguzi.
"Nasoma
maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali,
dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa
wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba
ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali
yaishe? Lipumba apewe kila kitu...hadi roho zetu, lakini misingi yetu,
misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo
silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile
anazozitizama msaliti" alisema Mtatiro na kuongeza;
"Ni
mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe
baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko
adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana
kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba"
Aidha
Mtatiro amesema kuwa ni rahisi sana kufanyakazi na Chama cha Mapinduzi
CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Ibrahim Lipumba kwakuwa alichokifanya
si kitendo cha kiungwana.
Julius
Mtatiro kwa sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo na ayasema
hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo
halitawezekana wao kukubali yaishe.
Post a Comment