Lipumba akwama kufuta kesi inayomzuia kupewa ruzuku ya CUF
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekataa maombi ya Mwenyekitti wa CUF
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim
Lipumba na wenzake, ya kufuta kesi namba 28/2017 inayomzuia kupata
ruzuku ya chama hicho.
Kupitia
taarifa yake kwa umma aliyotoa Agosti 17, 2017, Naibu Mkurugenzi wa
Habari, Mawasiliano na Umma CUF, Mbarala Maharagande amesema Jaji wa
Mahakama Kuu, Wilfred Ndyansobera anayesimamia kesi hiyo, amekataa
maombi hayo ya Lipumba ambaye ni mshitakiwa kwenye kesi hiyo.
Kwa
mujibu wa Maharagande, kufuatia maamuzi hayo ya mahakama, Prof. Lipumba
na wenzake watakosa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 ambazo zilikuwa
ruzuku ya chama hicho mpaka mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.
Kesi
hiyo ilifunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF inayomuunga mkono Katibu
Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad baada ya Lipumba kupewa
ruzuku ya chama hicho na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Ambapo
Bodi hiyo inadai kuwa uamuzi huo ulikuwa kinyume cha sheria kwa madai
kuwa Lipumba si kiongozi halali wa chama hicho.
Post a Comment