Kidoa Adaiwa kuwa Bonge, Apoteza Uwezo Wake wa Faragha
MSANII wa filamu ambaye ndiye The Ijumaa Sexiest Girl 2015, Asha Salum ‘Kidoa’ amegandwa na madai ya kuwa bonge nyanya tofauti na alivyokuwa huko nyuma kiasi cha kuathiri uwezo wake awapo faragha.
Akipiga stori mmoja wa mashosti wa staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, mara kwa mara Kidoa amekuwa akijilaumu kwa kushindwa kuukontroo mwili wake huku akihofia kuachwa na ‘baby’ wake.
“Unajua sasa hivi Kidoa amekuwa bonge sana na anahisi hata mpenzi wake atamuacha maana yale mambo ya chumbani atakuwa hayamudu,” alimwaga siri za chumbani za kidoa sosi huyo. Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kidoa na alipobanwa juu ya madai hayo alifunguka:
“Mh! Aliyewaambia hayo ni mmbeya sana, hata niwe bonge vipi bado siwezi kushindwa kujimudu faragha. Mimi ni msichana niliyefundwa, ni mtundu na mbunifu, hata mpenzi wangu anajua hilo. Kuhusu ubonge, nafanya jitihada za kurudisha ule mwili wangu na umbo namba nane,” alisema Kidoa.
Post a Comment