ad

ad

Jux Adaiwa Kupata Presha, Aanguka Sinza, Maeneo ya Legho

Mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Juma Musa maarufu kama Jux.

DAR ES SALAAM: Mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva, Juma Musa maarufu kama Jux, jana alijikuta akipandwa na presha na baadaye kuanguka, baada ya kukuta jengo ambalo ndani yake kuna duka lake la nguo, likivunjwa katika bomoabomoa iliyofanyika Sinza, maeneo ya Legho jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo iliyoangusha jengo ambalo zamani lilifahamika kama 92, dereva wa tingatinga lililobomoa, aliyekataa kujitambulisha, alisema miongoni mwa waathirika wa tukio hilo, ni pamona na Jux, ambaye alipokuta vitu vyake vimetolewa nje, akapatwa na masahibu hayo. 



A post shared by Juma_jux (@juma_jux) on
“Huyo Jux alipokuja na kuona vitu vyake vimetolewa nje, alivichukua, lakini ghafla presha ikampanda, akaanguka chini, watu wakamsaidia kumwingiza katika gari na kuondoka naye,” alisema mtu huyo. Risasi Mchanganyiko lilijaribu kumtafuta kwa simu muda mwingi jana, lakini simu yake haikupatikana hadi wakati likienda mtamboni. 

Mwathirika mwingine wa bomoabomoa hiyo, aliyejitambulisha kama Nabii John Bilionea, ambaye alikuwa na kanisa liitwalo Shalom, alisema amepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 250 na kwamba awali mmiliki wa jengo hilo, hakuwahi kumweleza kuwako kwa mgogoro. 

“Sikuwahi kuambiwa kama eneo hili lina mgogoro, tulikuwa na mkataba wa miaka minne na hadi leo imebaki miaka miwili, sijajua nini kitatokea kwa sababu itabidi tukae na mmiliki wakati mambo ya kisheria yakiendelea,” alisema. 

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio, zinasema mgogoro wa eneo hilo ulianza mwaka 2007, baada ya mmiliki wake wa awali, kutaka kuongezewa fedha zaidi ya makubaliano na mnunuzi. Katika kipindi chote hicho, jengo hilo lilikuwa likimilikiwa na mmiliki huyo wa awali na inadaiwa mnunuzi ndiye aliyeshinda kesi hiyo.

CREDIT: RISASI

No comments

Powered by Blogger.