ad

ad

INATISHA! WAUME ZA WATU WANAVYOIBIWA SALUNI DAR

HIVI NDIVYO WAUME ZA WATU WANAVYOIBIWA SALUNI
Kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa waume za watu kuibiwa bila kujielewa, kufanya uzinzi, usaliti na ngono katika baadhi ya saluni (Barber Shop), Kitengo cha Oparesheni fichua Maovu (OfM) kimefanya uchunguzi wa kina na kuibuka na ripoti ya kutisha ndani ya Jiji la Dar, Risasi Jumamosi limesheheni.

CHaNZO KILIVYOVUJISHA ISHU AwAlI


OFM ilizungumza na dada mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake ambaye alieleza namna ambavyo amebaini kwamba mumewe amemsaliti na chanzo kikubwa kikiwa kimeanzia kwenye saluni hizo. “Jamani nilinasa meseji za kimapenzi katika simu ya mume wangu, nikachukua ile namba na kumpigia na bahati nzuri yule dada alinipa ushirikiano mzuri na kunieleza kuwa anafanya kazi saluni za kiume na kwamba yeye anatafuta hela hivyo alimuingiza kingi wakati mwanaume huyo alipofika katika saluni yao,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

“Alikuwa mstarabu, akanielekeza jinsi wanavyowafanyia scrub, masaji katika saluni hizo na kuwafanyia vituko hadi kujikuta wakiomba namba ya simu na mambo mengine yanaanzia hapo.” OfM KaZiNi Mara baada ya kupata ubuyu huo, kwa takriban wiki mbili, makachero wa OFM walilazimika kutembelea saluni mbalimbali zilizopo maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke ambazo zinatoa huduma ya kunyoa, kufanya scrub, ‘stima’, pamoja na masaji ili kuweza kubaini yanayofanyika hadi baadhi ya wanaume wakijikuta wakisaliti ndoa na uhusiano wao.

MORI INAONGOZA KWA WELEDI

Katika maeneo ya Sinza-Mori, kwenye moja ya saluni, OFM ilibaini kuwa, huduma ya scrub, stima na masaji zinafanyika vizuri na warembo wanaofanya kazi katika saluni hiyo ni waaminifu na wanaifanya shughuli hiyo kwa weledi wake bila kuwashawishi wanaume wajikute wanapata vishawishi vya ngono. OFM iliwalipa wahudumu wa saluni hiyo na makachero wa OFM walinyolewa, wakapewa huduma ya scrub na stima bila kushawishiwa ngono.

KuiBiWa Ni KWa tOfauti OFM ilibaini kuwa, kuna waume za watu ambao wanachukuliwa kwa ridhaa yao baada ya kushawishiwa kwa huduma wanayofanyiwa, hususan kushikwashikwa sehemu ‘tatanishi’ kama kifuani, shingoni, kichwani na masikioni.

Kutokana na kushikwa huko, wanaume wanajikuta wakitoa hela nyingi zaidi ya shilingi elfu hamsini hadi laki kwa kukubali kufanyiwa huduma nyingi baada ya kunyoa ikiwemo masaji, scrub na stima ambapo kila huduma inakuwa na bei yake.

GHARAMA ZaO OFM

ilibaini kuwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar, bei wanazopewa wateja hazitofautiani sana japo makubaliano mengine yanayosababisha waume za watu wasaliti ndoa zao, hufanyika kati ya mteja na warembo wanaotoa huduma hizo.

WENGINE WANAMALIZA HAPOHAPO

Uchunguzi huo ulibaini, kuna baadhi ya wanaume za watu wanashawishiwa na wadada hao wa saluni na kujikuta wakifanya ngono ndani ya baadhi ya saluni ambazo zina vyumba maalum vya kufanyia masaji hizo. WENGiNE WaNaSuBiRi Off OFM ilibaini pia, wapo baadhi ya wanaume ambao wakishashawishiwa na wadada hao, wanaomba namba za simu kisha kwenda kumalizia mambo yao katika nyumba za kulala wageni siku ambazo warembo hao hawaendi kazini (off).

BEi ZaO SaSa Uchunguzi wa OFM ulizidi kubaini kuwa, bei rasmi elekezi za kupewa huduma hizo ni kama ifuatavyo: Kunyoa na scrub ni kati ya shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano. Masaji ya mwili mzima ni kati ya shilingi elfu hamsini hadi sitini. Masaji ya nusu mwili ni kati ya shilingi elfu ishirini hadi thelathini.

WaNaOJiuZa OFM

ilibaini baadhi ya warembo wanaofanya kazi katika saluni hizo wapo ambao wanatangaza dau la kujiuza mapema kwa mteja kati ya shilingi elfu ishirini na tano hadi hamsini na ukionekana ‘wa kuja’ unapigwa pesa ndefu.

WaPO WaNaOfaNYa KWa WELEDi OFM

ilifanya uchunguzi katika baadhi ya saluni na kubaini warembo hao ambao kuna wenye wapenzi na waume zao wanafanya kazi kwa weledi bila kuwashawishi wanaume hao waingie mkenge.

“Sisi hapa tunafanya kazi yetu kwa weledi sema kuna wenzetu ndio ambao wanazidisha mbwembwe kwa mteja hadi anajikuta akisaliti ndoa yake ingawa pia huwezi kuwalaumu kwani hata hao waume za watu huwa wanapenda kufanyiwa hivyo,” alisema mmoja wa warembo anayefanya kazi ya saluni maeneo ya Sinza alipohojiwa na OFM.

WaMiLiKi HaWaWEZi KuDHiBiti Uchunguzi umebaini, hata wamiliki wa saluni hizo, wengi wao wanasimamia kwa weledi japo wanashindwa kudhibiti baadhi ya warembo wanaowashawishi waume za watu kwani makubaliano ya usaliti hufanyika kwa siri katika chumba cha kufanyiwa usafi baada ya kunyolewa.

Hata hivyo, wengi wao wanawakabidhi vijana wa kiume kunyoa na wao jioni kuchukua tu hesabu ya siku hivyo kutojua kwa undani yanayofanyika ndani ya saluni zao.

UfafaNuZi PiCHa Za MBELE

Picha zote zilizotumika katika ukurasa wa mbele hazihusiani kabisa na warembo ambao wanafanya huduma isiyokuwa na weledi. Zimepigwa maalum kuonesha uhalisia wa tukio.

NENO LA MHARIRI

Ni vyema wenye waume wakajitambua, wakajiheshimu kwani suala hilo linahusu tabia ya mtu mmojammoja. Kama umeingia kwenye ndoa au una mpenzi wako, huna sababu ya kushawishika kirahisi pindi unapopewa huduma hiyo na kama unaona huwezi kuhimili, ni bora usifanye kabisa au ukafanyiwe na mkeo.

CHANZO: RISASI JUMAMOSI

No comments

Powered by Blogger.