Alichokisema Tundu Lissu Leo Hoteli ya Protea, Dar
MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Tundu Lissu, leo ameongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam akisindikizwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederick Sumaye ambapo miongoni mwa mambo mengi aliitaka serikali kufafanua juu ya mambo kadhaa.
Aliitaka serikali kuelezea kuhusu ndege ambayo ilitakiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu ambapo hadi sasa haijafika. Kwa mujibu wa Lissu, alitaja sababu za kutofika kwa ndege hiyo ambayo ni kukamatwa ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 kwa sababu Tanzania inadaiwa fedha na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd ambayo iliomba kibali na kupewa kutoka Mahakama Kuu ya Montreal kukamata mali zozote za Tanzania zitakazokuwa nchini Canada.
Lissu aliyasema hayo na kusisitiza kwamba serikali na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa hajasema lolote kuhusu suala hilo.
Miongoni mwa mambo mengine aliyoyasema ni kuvitaka vyombo vya dola kufanya kazi zake inazotakiwa kwa maslahi ya taifa na si kwa kuwafuatilia watu wasiokuwa na hatia, hususani wanasiasa.
"Serikali ilisema moja ya ndege ilizoagiza, ingewasili Tanzania Julai 2017,mpaka sasa haijawasili, iko wapi? " - @Tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/6LRAGvsKbg
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Kutokana na ndege hiyo ya Bombadier kutowasili Tanzania kama ilivyoahidiwa, Serikali imepatwa na kimya cha ghafla" @tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/9zdiGTpWpe
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Profesa Mbarawa hajasema ukweli, Bombadier ya Magufuli imekamatwa na inashikiliwa Canada na wadeni wake" @tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/79qAaCeT9M
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Prof. @MbarawaM hajasema kilichosababisha ndege ya Bombadier isiwasili TZ Julai 2017 kama ilivyoahidiwa hapo awali" @tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/gZUEY4Snvz
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Suala la kukamatwa kwa Bombadier ya Magufuli linaibua maswali mengi yanayohitaji majibu ya Rais na Serikali yake" @Tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/NhylzNnAod
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Dkt. Mahiga alifanya ziara Canada,akiwa na Balozi wa TZ Canada,Jack Zoka,walifanya mazungumzo na Stirling Civil Engineering Ltd #PRESSLEO pic.twitter.com/2CbpbpUHcY
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Mazungumzo yao yalihusu deni la USD 38,711,479 inayodaiwa TZ kutokana na hukumu 2 za Mahakama ya Usuluhishi zilizotolewa 2009/10 #PRESSLEO pic.twitter.com/3XIyx5I5xd
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Mazungumzo hayo pia yalihusu amri ya kukamatwa mali zote za TZ zilizopo mikononi mwa kampuni ya kutengeneza ndege ya Bombadier @Tundulissutz pic.twitter.com/UFFzQuhUfu
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Mnamo 10 Desemba 2009 na baadae 10 Juni 2010, Mahakama ya usuluhishi ilitoa tuzo ya USD 25M na riba 8% hadi malipo yatakapofanyika #PRESSLEO pic.twitter.com/YlE8zMuYCa
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Kutokana na ucheleweshwaji wa malipo kwa Stirling Civil Engineering Ltd,deni limeongezeka hadi USD 38,711,479 kufikia 30/7/2017 #PRESSLEO pic.twitter.com/4MJLHf34VI
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Amri ya Mahakama Kuu ya Montreal ya kukamata mali za zote za Tanzania ni pamoja na ndege ya Bombadier Q400" @Tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/dYpznVEWQm
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Sasa tunataka kujua nani atakayewajibika kijinai kwa kulisababishia Taifa hasara ya sh. 87bn iliyopelekea mali zetu kukamatwa" Tundulissutz pic.twitter.com/mQ14rjbypW
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Kwanini deni la Stirling Civil Engeering Ltd,halikulipwa mara baada ya Mahakama ya usuluhishi kutoa tuzo ya USD 25M hadi kufikia USD 38.711? pic.twitter.com/ETcvnRl0Ae
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Msisitizo wa Waziri Mahiga kwamba suala hili lifanywe kwa siri lisitangazwe unalenga kumlinda nani na kwa nini? " @Tundulissutz #PRESSLEO pic.twitter.com/OaUM60gyK1
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
"Katiba hii kama alivyosema Mw. Nyerere, Inampa Rais mamlaka ya kidikteta,ni muhimu kurejesha mjadala wa Katiba Mpya na Demokrasia" -Lissu pic.twitter.com/XAveTTKZZu
— CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) August 18, 2017
Post a Comment