Wajumbe Wa Kamati Ya Uchaguzi Wampinga Mwenyekiti Wao, Watengeneza Njia Malinzi Afanyiwe Usaili
Wajumbe
wa kamati ya uchaguzi ya TFF, wameonyesha wazi wao wanataka kubadili
utaratibu sahihi wa kamati hiyo ili kutoa nafasi wagombea walio mahabusu
nao kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi.
Jamal
Malinzi anayegombea urais kutetea kiti chake na Geofrey Nyange ‘Kaburu’
anayewania makamu mwenyekiti wapo mahabusu wakituhumiwa na makosa
mbalimbali yakiwemo ya utakatishaji fedha.
Lakini
watu wa kamati hiyo wameonekana kutofautiana baada ya mwenyekiti
kusisitiza, kesho ndiyo mwisho wa usaili na ambaye hatatokea kama kanuni
zinavyosema zinaeleza atakuwa amejitoa katika uchaguzi.
Wajumbe wameonekana kumpinga mwenyekiti wakitaka ufanyike usajili hata wa kuandika tu.
Maana
yake walio mahabusu wanaweza kuandika barua na kujieleza na usaili
ukafanyika jambo ambalo linaonekana kupindisha utaratibu.
Awali, mwenyekiti alifanya kikao na waandishi wa habari leo mchana na kusema wazi sahihi ni anayekosa usaili anakuwa amejiondoa.
Alipoondika,
wajumbe nao wakafanya mkutano na waandishi. Hawakuonyesha wanampinga
mwenyekiti lakini wakasisitiza kuwa usaili unaweza kufanyika kwa
maandishi au hata baada ya siku tatu zilizotangazwa za usaili.
Post a Comment