Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imewateuwa 8 kuwa Wabunge wa Viti Maalumu CUF
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 27 Julai 2017imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF).
1- Ndugu Rukia Ahmed Kassim;
2- Ndugu Shamsia Aziz Mtamba;
3- Ndugu Kiza Hussein Mayeye;
4- Ndugu Zainab Mndolwa Amir;
5- Ndugu Hindu Hamis Mwenda;
6- Ndugu Sonia Juma Magogo;
7- Ndugu Alfredina Apolinary Kahigi; na
8- Ndugu Nuru Awadh Bafadhili,
Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa nafasi waza nane (8) za Wabunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF.
Post a Comment