Mwana FA na AY Waendelea Kutamba Mahakamani
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya Kampuni hiyo ya
huduma za simu za mkononi iliyotaka kukata rufaa katika Mahakama ya
Rufaa kupinga amri ya kutakiwa kuwalipa wasanii hao kiasi hicho cha
fedha.
Hivi
karibuni, Mahakama Kuu ilihalalisha uamuzi wa Mahakama ya Wilaya
iliyoikuta na hatia ya kutumia bila kibali nyimbo za wasanii hao kama
miito ya simu na kuitaka kuwalipa kiasi hicho cha fedha.
Wakili
wa wasanii hao, Albert Msando aliweka pingamizi akiiomba Mahakama Kuu
kuyakataa maombi yaliyowasilishwa na wanasheria wa kampuni ya Mic kwa
madai kuwa ni batili kwani yalikuwa na makosa ya kisheria.
Jaji
Isaya Arufani wa Mahakama Kuu alikubaliana na maelezo ya Wakili Msando
na kuyatupilia mbali maombi ya wanasheria wa kampuni hiyo. Bado
haijafahamika kama watafanya marekebisho na kurejesha maombi mapya au
la.
AY na Mwana FA wanadai kuwa kampuni ya Mic Tanzania Limited ilitumia bila ruhusa yao nyimbo zao ‘Usije Mjini’ na ‘Dakika Moja’.
Post a Comment