Lucy Komba Atamani Mwanaye Angekuwa Mzungu
MSANII wa filamu Lucy Komba amesema, anajivunia kuona mtoto wake anayeishi naye nchini Denmark kwa mumewe, kuweza kuongea lugha ya Kingereza na kusahau kabisa Kiswahili.
Akipiga Stori na 3-Tamu, Lucy alisema moja ya vitu vilivyomfanya akaishi huko na mwa naye ambaye si mtoto wa Mzungu huyo ni kutaka awe na tabia za Kizungu ikiwemo kujua lugha hiyo kwa ufasaha ili kuondokana na mambo mengi ya Kiswahili, ikiwemo kumsomeshe nchi za Wazungu hadi pale atakapohitimu elimu ya juu.
"Kitambo nawaza malezi bora kwa mwanangu, sikupenda awe na tabia za Kibongo japo ni Mbongo, hivi sasa siyo yeye kabisa ameshasahau Kiswahili siku nyingi maana mtoto ananasa kirahisi, nimefurahi mno," alisema Lucy ambaye mtoto wake anayeitwa Strom anaishi naye huko zaidi ya mwaka sasa.
Post a Comment