Mke wa Rais Mugabe Amtaka Mumewe Kumtangaza Mrithi Wake
Mke wa Rais wa Zimabwe, Robert Mugabe, Bi. Grace Mugabe amemtaka kiongozi huyo kumtangaza mrithi wake wa urais ili kuondoa minong’ono kuhusu mtu atakayemrithi akiondoka madarakani.
”Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno lake litakuwa la mwisho”, alisema Bi Grace Mugabe.
Rais Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi duniani na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyingine mwaka ujao.
Lakini makundi ya wapinzani yamekuwa wakijipanga kuwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment