Jaap Stam Beki Kisiki Ambaye Ferguson Alijuta Kumuuza
Mholanzi mwenye sura ya kikatili uwanjani, Jaap Stam.
JAAP Stam alikuwa ni Mholanzi mwenye sura ya kikatili uwanjani na alishiriki kwa kiasi kikubwa kuipa Manches¬ter United ubingwa wa Ligi Kuu England mara tatu mfululizo kuanzia 1999, 2000 na 2001.
Stam ambaye jina lake kamili ni Jakob “Jaap” Stam, aliyezaliwa Julai 17, 1972, katika maisha yake ya takriban miaka 15 kwenye soka, alifanikiwa kupa¬ta medali kibao zikiwemo binafsi kutokana na juhudi kubwa alizokuwa nazo uwanjani.
JaaP Stam enzi akiwa Manchester United.[/caption]Pamoja na mataji kibao, Stam alipata tuzo nyingi ikiwemo ya kupigiwa kura kuwa Beki Bora wa Ligi ya Mab¬ingwa Ulaya msimu wa 1998- 99 pamoja na 1999-2000.
Lakini Stam pia alikuwemo katika kikosi cha Manchester United kilichoishangaza dunia kwa kusawazisha na kufunga bao la ushindi kilipokuwa nyu¬ma kwa bao 1-0 dhidi ya Bayern Munich hadi dakika ya 90 katika fainali ya Ligi ya Mab¬ingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona Mei 26, 1999.
...Akijiandaa kupiga mpira.Beki huyu wa kati aliyekuwa na mwili mkubwa, imara na mwenye nguvu nyingi asi¬yetaka masihala katika kazi, alikuwa na mbinu nyingi, kasi na maarifa. Aliweza pia kuche¬za kama beki wa pembeni.
Katika kikosi cha timu ya tai¬fa ya Uholanzi, Stam alicheza mechi 67 na kufunga mabao matatu kuanzia 1996 hadi 2004. Alikuwemo katika kikosi cha Uholanzi kwenye michuano mitatu ya Ulaya (Euro) na Kombe la Dunia 1998.
Lakini ni katika kikosi cha Manchester United ndiko umaarufu wake ulipokuwa mkubwa zaidi, kwani aliiwezesha kutwaa mataji matatu ya Premier, Kombe la FA, Intercontinental Cup na Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
JaaP Stam alipata tuzo nyingi sana.[/caption]Alifunga bao lake pekee klabuni hapo katika ushindi wa ugenini wa mabao 6-2 dhidi ya Leicester City.
Mapema msimu wa 2001– 02, Stam ghafla aliuzwa bila kutarajia na Sir Alex Ferguson kufuatia kocha huyo kudaiwa kukerwa na tuhuma ambazo Stam alidaiwa kuzitoa dhidi yake na klabu katika kitabu.
Hata hivyo, mwaka 2007, Ferguson alitamka kuwa ali¬fanya kosa kubwa kumuuza Stam.
Stam akiichezea AC Milan, alikuwemo katika kikosi cha kihistoria kilichopoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool baada ya kutan¬gulia kufunga mabao 3-0 hadi mapumziko lakini Liver waka¬yarudisha na mwisho wa siku wakashinda kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Stam alitangaza kustaafu kucheza soka Oktoba 29, 2007 akiwa na umri wa miaka 35. MATAJI
Akiwa PSV:
Ubingwa Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie): 1996–97
Ubingwa KNVB Cup: 1995– 96
Johan Cruyff Shield: 1996, 1997
MA N C H E S T E R UNITED:
Premier League (3): 1998– 99, 1999–2000, 2000–01
FA Cup (1): 1998–99
Ligi ya Mabingwa Ulaya (1): 1998–99
Intercontinental Cup (1): 1999
LAZIO:
Coppa Italia (1): 2003–04
MILAN:
Supercoppa Italiana (1): 2004
AJAX:
KNVB Cup (1): 2006–07
Johan Cruijff-schaal (2): 2006, 2007
T U Z O BINAF¬SI:
M w a ¬n a s o k a Bora wa Mwaka Uholan¬zi (1): 1997
K i a tu cha D h a ¬h a b u Uh o l a n z i (1): 1997
Beki Bora wa Klabu za Uefa (2): 1998–99, 1999–2000
MAISHA BINAFSI
Tangu mwaka 1997, Stam a m e m u o a mrembo Ellis Stam na wana watoto wanne ambao ni Jake Stam, Megan Stam, Lisa Stam na Thomas Stam. Familia ya Stam inaishi jijini A m ¬sterdam, Uholanzi, wakati yeye yupo mjini Reading, Eng¬land akipiga kazi.
ANACHOKIFANYA KWA SASA
Oktoba 2008, Stam alire¬jea Manchester United akiwa skauti wa klabu hiyo. Lakini tangu mwaka 2011 alianza maisha ya ukocha. Al¬ianza kwa kuwa Ko¬cha Msaidizi wa PEC Zwolle ya Uholanzi kwa misimu mi¬w i l i . B a a d a y e a k awa K o c h a Msaidizi wa Ajax kwa miaka mitatu, na kuanzia msimu wa 2013-14 akawa kocha wa mabeki wa timu hiyo. Kuanzia Juni 13, 2016, Stam aliteuliwa kuwa Kocha wa Read¬ing inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza England ‘Champi¬onship’. Nusu¬ra aipandishe timu hiyo daraja msimu uliopita lakini il¬ifungwa kwenye ‘playoffs’.
KLABU ALIZOCHEZEA MWAKA KLABU MECHI MABAO
1992–1993 FC Zwolle 32 1
1993–1995 Cambuur 66 3
1995–1996 Willem II 19 1
1996–1998 PSV 76 12
1998–2001 Man U 127 1
2001–2004 Lazio 70 3
2004–2006 Milan 65 2
2006–2007 Ajax 31 1
Jumla 486 24
Post a Comment