YANGA YATOA KAULI KUHUSU KUPIGWA BAO KWENYE USAJILI, KISA NI SIMBA, AZAM FC
Yanga imeweka wazi mipango yake ya usajili kuwa itafanya taratibu na umakini mkubwa na siyo kukurupuka.
Kauli hiyo imekuja baada ya kuonekana kuwa Yanga imekuwa nyuma katika suala la usajili ikiachwa na wapinzani wao wa jadi, Simba pamoja na Azam FC.
Klabu ya Yanga, imeweka wazi mipango yake ya usajili kuwa itafanya taratibu na umakini mkubwa na siyo kukurupuka kama ilivyo kwa baadhi ya timu nyingine.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa amesema wanaheshimu usajili kwa sababu ndiyo unaoweza kuwapa mafanikio hivyo hawawezi kukurupuka na kugombania wachezaji wakati wanamuda mrefu wa kufanya zoezi hilo.
"Tunachofanya kwa sasa ni kuangalia mahitaji ya kikosi chetu kwa msimu ujao tunafanamu kuwa tutashiriki ligi ya mabingwa kwaiyo lazima tuwe na kikosi imara mabacho kitaweza kutufikisha mbali tofauti na miaka iliyopita," amesema Mkwasa.
Katibu huyo amesema tatizo la kimya chao siyo pesa bali ni kutafakari kwa makini ni namna gani ya kuanza kuifanyia kazi ripoti yaliyoiacha kocha wao George Lwandamina na kufanikiwa kwa kila walichokikusudia.
Amesema mpaka sasa zoezi lao linakwenda vizuri na hakuna kitakachoharibika hadi na anaimani Yanga itakuwa na kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri msimu ujao na kutetea mataji yake yote iliyowahi kuyatwaa misimu uliyopita.
Mkwasa amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu kwani uongozi wake unajua unachokifanya na baada ya muda mfupi kila kitu kitakuwa sawa ikiwemo na kusajili wachezaji nyota watakaoipa mafanikio timu hiyo.

Post a Comment