Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa
ameipongeza Vodacom Tanzania Foundation kwa kuendelea kuwafuturisha
watoto na wazee waishio katika mazingira magumu nchini. Mh. Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Kassim(katikati)
akishuhudia Shekh mkuu wa Ruangwa mkoa wa Lindi akipokea boksi lenye
tende kwa niaba ya watoto wanaoshi katika mazingira magumu mkoani hapo
toka kwa Meneja mauzo wa mkoa huo,Omary Kilumanga na Mkuu wa kitengo cha
Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu baada ya
kufuturu futari mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania
Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani. Mh. Waziri Mkuu ameyasema hayo mwishoni mwa wiki
iliyopita mjini Ruangwa Lindi katika futari iliyoandaliwa na Vodacom
Tanzania Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika
mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Kassim akiongea
na wakazi wa Ruangwa mkoa wa Lindi mara baada ya kufuturu futari
mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania Foundation mkoani
humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Mtazame Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Pwani wa Vodacom Tanzania Plc,
Aileen Meena akifafanua kampeni mpya "Ukarimu wa Vodacom" katika msimu
huu wa Ramadhan.
Huu ni
mwendelezo wa kampeni ya “Ukarimu wa Vodacom” ambayo ina lengo la
ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na
katika maisha ya kila siku. Huduma hii yenye lengo la kuendeleza
mshikamano inakwenda sambamba na kuwawezesha Waislamu na Watanzania kwa
ujumla wao kujiunga na kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na
kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku,
kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa
kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii
mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo
wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu
kwa siku 7.
Post a Comment