STAA wa
Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anadaiwa kulelewa na
mwanamama ambaye ni msanii wa filamu wa zamani, Muna Alphonce ‘Munalove’
na sasa wanapika na kupakua.
Msanii wa filamu wa zamani, Muna Alphonce ‘Munalove’.
Chanzo makini kiliiambia Risasi Vibes
kuwa, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi ambapo ukaribu
huo unaonesha kwamba ni wapenzi na inasemekana mwanamama huyo ambaye
amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mwanamuziki Kalala Junior ndiye
anayemfanya msanii huyo kuonekana akipigilia nguo za thamani tofauti na
zamani.
Muna Alphonce ‘Munalove’.
Baada ya kupata habari hizo, Risasi Vibes iliwatafuta
wawili hao ambapo majibu yao yalionesha kujichanganya na kuzua
sintofahamu zaidi kwani Dogo Janja alikanusha kwamba siyo kweli na
hamfahamu kabisa mwanamama huyo. Upande wa Muna alisema; “Dogo Janja ni mdogo wangu sana na ninamchukulia hivyo siyo mpenzi wangu jamani.” STORI: RISASI VIBES | RISASI MCHANGANYIKO
Post a Comment