Kauli ya Yanga Kuhusu Kuondoka kwa Niyonzima

TAARIFA KWA UMMA
Yanga
SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha
wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda
Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo
katika kiwango cha juu.Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.
Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo Young Africans Sports club. 21-06-2017.
Post a Comment