Mdee, Bulaya Wasimamishwa Kuhudhuria Bunge Hadi Mwaka 2018
DODOMA:
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya wote
wa CHADEMA wameadhibiwa kwa kusimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao
vyote vilivyosalia vya mkutano wa 7 wa Bunge la Bajeti linaloendelea
hivi sasa mjini hapa, pia hawatohudhuria mkutano wa 8 na wa 9 kwa utovu
wa nidhamu
Aidha Bunge limeamua kuwa, wabunge hao watarudi kuhudhuria vikao kuanzia kwenye Bunge la Bajeti mwaka ujao (2018/2019).
Tukio
hilo limeibuka kufuatia vurugu zilizoibuka Ijumaa iliyopita baada ya
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde kudai kwamba wapinzani bungeni
humo wanatetea wezi wa mchanga wa dhahabu, hali iliyosababisha Mbunge wa
Kibamba, John Mnyika kuibuka na kubishana. Mbunge mwingine ambaye
hakujulikana jina lake aliwasha maiki na kumuita Mnyika mwizi, Mnyika
alikitaka kiti cha Spika kimuamuru mbunge huyo kufuta kauli yake lakini
spika alisema hakumsikia aliyesema maneno hayo.
Baada ya mabishano kati ya Spika na Mnyika, spika aliamuru Mnyika atolewe nje na polisi wa Bunge, hali iliyosababisha Halima Mdee na Ester Bulaya, waiingilie kati kuwazuia askari hao kumtoa nje. Jambo hilo lilisababisha tafrani licha ya Mnyika kutolewa nje huku wabunge wa upinzani wakitoka nje.
Spika alitangaza kumsimamisha Mnyika asihudhurie vikao vya bunge kwa wiki moja huku akisema Ester Bulaya na Halima Mdee wataandikiwa barua ili wakahojiwe na Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge ambapo leo wameadhibiwa wasihudhurie vikao vya bunge kama ilivyoelezwa hapo mwanzo.
Aidha Bunge limeamua kuwa, wabunge hao watarudi kuhudhuria vikao kuanzia kwenye Bunge la Bajeti mwaka ujao (2018/2019).
Hukumu
hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo. Mapema
leo, Jumatatu Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu
za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.
Hata
hivyo, Bunge liliendelea kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na
Kawe. Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge
kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.
Kanuni
inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria
vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa
kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

Post a Comment