Mbowe Aikana Sauti Inayosambaa Mitandaoni Ikidai Wema Sepetu ni Mpenzi Wake
Habari
inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio (voice
note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai
Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.
Jana kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM Mbowe ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka:
“Mimi
nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa
ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema
kwa sababu siyo za kweli.
“Timu
yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo
limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na
ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.
"Sauti
siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni
mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za
upotoshaji tu."
Post a Comment