Kidoa: Sina Ndoto za Kuwa Mwanamuziki Maishani Mwangu
MUUZA nyago anayefanya poa kwenye video mbalimbali nchini ‘Kidoa’ amesema kuwa hana mpango wa kuingia kwenye muziki kama wafanyavyo video queens wengine kwa sababu hana kipaji cha kuimba.
Akibonga na Mikito Nusunusu, Kidoa alieleza kuwa ingawa anapenda muziki lakini hana mpango wa kuingia kwenye fani hiyo kama wenzake kwani hajui kuimba na hajawahi kutamani kuwa mwanamuziki hivyo akilazimisha kuingia atachemka.
“Napenda niendelee kuwa video queen na siyo zaidi ya hilo, sina mpango wa kuwa mwanamuziki na siwezi kutamani fani hiyo acha nibaki huku na nina furaha na hiki nikifanyacho ndiyo maana unaona nafanya vizuri kwenye video mbalimbali,” alisema Kidoa.
Na Ally Katalambula | RISAI JUMAMOSI
Post a Comment