ad

ad

Droo Ndogo Ya Nne Shinda Nyumba: Washindi Wa Ving’amuzi Vya Ting Kwatu!

DAR ES SALAAM: Baada ya washindi wa watatu wa droo ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya pili kupewa zawadi zao Jumanne, juzi walioshinda ving’amuzi vya Ting, ambao ni watano, nao walikabidhiwa chao katika hafla itakayofanyika katika ofisi za Global Publishers, Bamaga Mwenge jijini Dar.
Mwakilishi wa TING, Caroline Collent (kushoto) akimkabidhi zawadi ya King’amuzi, Ally Ramadhani Kazi.
Washindi hao walikabidhiwa zawadi hizo baada ya Peter Christopher Katua wa Ilala jijini Dar, kushinda seti ya vyombo (dinner set), Ally Halifa Kachenje wa Arusha (simu) na Shabani Ahmadi Ngao wa Tabata Dar aliyeibuka mshindi wa pikipiki kupewa chao.
Washindi wa juzi waliokuwa wachukue chao walikuwa ni Dokta Uhemba (Dodoma) Verus Kweyamba (Moshi) Ally Ramadhan (Mburahati), Rhoda Kimenyi wa Morogoro na Ringo Mbuya mkazi wa Uyole mkoani Mbeya.
Mwakilishi wa TING, Caroline Collent (kushoto) akimkabidhi zawadi ya king’amuzi, Farida Mukhisin aliyekua kwa niaba ya Verus Kweyamba wa Moshi.
Hata hivyo, ni washindi watatu tu ndiyo waliojitokeza na kupewa zawadi zao, ambao ni Ally Ramadhan Kazi, Verus Kweyamba na Rhoda Kimenyi. Ambao hawakutokea ni Dokta Uhemba na Ringo  Mbuya ambao utaratibu mwingine utafanyika juu ya kupewa zawadi zao.
Afisa Masoko wa Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda, Yohana Mkanda, alisema zoezi hilo limehitimisha shughuli za droo ndogo ya nne, iliyofanyika wiki mbili zilizopita katika viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar.
Mkuu wa Idara ya Usambazaji ya Global Publishers, LawranceKabende akimkabidhi zawa ya King’amuzi cha TING, Mary Mboya aliyechukua kwa niaba ya RhodaKimenyiwa Mrogoro.
“Hapa sasa tumekamilisha zoezi letu kuhusu droo ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, niwaombe wasomaji wa magazeti yetu kuendelea kutuunga mkono kwa kununua na kujaza kuponi na kuzituma kwetu kupitia mawakala wetu walio nchi nzima, kama kuna tatizo la namna ya kuwapata, tafadhali wawasiliane nasi kupitia namba zinazopatikana kwenye magazeti yetu yote kwa maelekezo zaidi,” alisema Mkanda.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.
Na Mwandishi Wetu

No comments

Powered by Blogger.