Msanii wa muziki hip hop kutoka Tiptop Connection, Dogo Janja.
MSANII
wa muziki hip hop kutoka Tiptop Connection, Dogo Janja, ambaye kwa
sasa anafanya vizuri na ngoma yake inayoitwa Utavaaje? amefunguka mengi
juu ya ngoma yake ya kitambo kidogo inayoitwa Binadamu aliyomshirikisha
PNC Shino kwamba mwimbaji Darassa amehusika kuandika ngoma hiyo ya
Binadamu.
Msanii wa bongo fleva, Darassa.
Darassa
ameshiriki sehemu kubwa kwenye ngoma hiyo ambayo Dogo Janja alikuwa
katika usimamizi mpya wa Watanashati kwani hata anavyoimba hiyo ngoma ni
kama Darassa kabisa. Alivyoulizwa na Dullah wa kipindi cha Planet
Bongo cha kituo cha televisheni cha EATV kuhusu aliyeiandika ngoma
hiyo, alisema Darassa alihusika kwenye uandishi wake kwa aslimia 80.
Post a Comment