Bajeti: Serikali yafuta ushuru wa gesti .....Yatangaza Neema Kwa Wafanyabiashara
Hayo
yameelezwa leo (Alhamisi) bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk
Phillip Mpango wakati akiwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18.
Pamoja
na ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza
mahali zinapopatikana huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.
Katika
hatua nyingine, Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa
vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.
Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.
Post a Comment