Bajeti: Road License yafutwa, sasa kulipwa mara moja
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.
Amesema
uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari
linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa
katika mafuta ya petroli na dizeli.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.
Pamoja
na hayo, Waziri Mpango ameshuha ushuru kwa mvinyo unaotengenezwa kwa
zabibu zinazozalishwa ndani kutoka Sh202 kwa lita hadi Sh200 kwa lita.
Kadhalika ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Sh429 hadi 450 kwa lita.
Wakati huo, ushuru wa bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka Sh534 hadi Sh564 kwa lita.
Post a Comment