ad

ad

Ajibu Atua Yanga Kwa Kishindo, Mashabiki wa Simba wabaki Mdomo wazi

 
HUU sasa unaitwa mwendo wa piga ngumi nikutwange konde, umwamba katika usajili unazidi kuendelea katika soka la Tanzania, ubabe kwa asilimia kubwa unafanywa na Klabu za Simba, Yanga na Azam FC. Habari ikufikie kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga umefikia makubaliano mazuri na kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu na tayari amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili Jangwani lakini kuna kitu kuhusu mkataba huo. 

Taarifa hizo zimekuja wakati ambapo kuna madai kuwa Mwenyekiti Yusuf Manji ambaye aliandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo, amerejea kimyakimya kwa kutia mkono katika usajili wa Yanga ambao ulionekana kusuasua katika siku za hivi karibuni huku Simba na Azam FC zikitamba kwa kusajili wachezaji waliotamba msimu uliopita. 

Pamoja na taarifa hizo, uhakika ni kuwa Manji hajabadili uamuzi wake wa kutoka kwenye kujiuzulu lakini usajili wa Ajibu umekuja muda mfupi baada ya Yanga kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Jang’ombe Boys, Abdallah Haji Shaibu. Ajibu ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye orodha ya nyota wanaowaniwa vikali na Yanga katika msimu ujao wa ligi kuu.

 Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Ajibu ni mchezaji wa kwanza kupendekezwa kusajiliwa na Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina lakini mpango ulikuwa ukikwama kutokana na kutokamilika kwa mazungumzo baina yao na mchezaji huyo. Mtoa taarifa huyo alisema katika kuhakikisha wanafanikisha mapendekezo ya kocha huyo, uongozi wa timu hiyo jana asubuhi ulifanikisha usajili huo kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili lakini hawawezi kuuweka wazi hadi mwezi ujao atakapomalizana kabisa na Simba. Aliongeza kuwa, bado wanaendelea kuifanyia kazi ripoti
WAKATI Yanga wakimsubiria kiungo wao mchezeshaji, Haruna Niyonzima atue nchini kwa ajili ya kumuongezea mkataba watani wao wa Simba wenyewe hawakauki Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ili wamsainishe.


 Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu tetesi zienee kuwa kiungo huyo anayemudu kucheza namba nane tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba. Kiungo huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kutokana na mkataba wake kumalizika mwezi ujao kwa mujibu wa kanuni za Fifa. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka kwa ndugu wa karibu wa Niyonzima viongozi wa Simba walikuwa tayari wapande ndege kumfuata kiungo huyo Rwanda, lakini ilishindikana kutokana na kukatishwa tamaa na meneja wake. Mtoa taarifa huyo, mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ ndiye alikuwa anawasiliana na Niyonzima kwa ajili ya kwenda kumsainisha nchini Rwanda kwa dau la shilingi milioni 70.

 “Nikwambie ukweli tu, ni ngumu Niyonzima kwenda kusaini mkataba wa kuichezea Simba, kwani mpango wao wa kwanza walioupanga umeshindikana kwani walipanga wamfuate Rwanda alipokuwa kwenye majukumu yake ya timu ya taifa. “Mipango hiyo ilishindikana ni baada ya meneja wake kuuzuia uongozi wa Simba usiende huko na badala yake wamsubirie hadi ataporejea nchini na baada ya kuona wamekwama, viongozi hao wa Simba wakaanza kwenda kumwinda uwanja wa ndege kwa kukagua muda wa ndege wa Rwanda Air na mratibu wa hilo ni Mo. “Lakini wakati wakipanga hayo, Bin Kleb (Abdallah), yeye aliwasiliana na Niyonzima na kumwambia mara baada ya kutua nchini asionane na yeyote zaidi yake yeye,” alisema mtoa taarifa huyo. 

Championi Ijumaa, lilimtafuta Niyonzima na kuzungumza naye moja kwa moja kutoka Rwanda kuhusiana na taarifa za yeye kusaini Simba alisema kuwa: “Hayo maneno tu wanaongea, nikuhakikishie mimi sijasaini Simba na kama unakumbuka mimi nilikwambia nimeichezea kwa amani Yanga miaka sita hivi sasa.”
ya kocha wa timu hiyo kwa kusajili wachezaji wote ambao amewapendekeza katika msimu ujao. “Kiukweli kabisa tumefikia makubaliano mazuri na Ajibu kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili Yanga, hivyo uongozi umemalizana naye kwa kuingia makubaliano ya miaka miwili. “Ajibu tumemsainisha baada ya kocha mwenyewe kumhitaji na kumuweka kwenye ripoti yake ya usajili, kiukweli ni kati ya wachezaji anaowakubali. 


“Uongozi umeshindwa kuweka wazi kila kitu kwenye usajili wake Ajibu kwa kuhofia kilichotokea kwenye usajili wa Kessy (Hassan) ambaye tulimsajili akiwa amebakisha wiki mbili na kusababisha kupigwa faini ya shilingi milioni 50, hivyo hawataki kitokee hicho tena, hivyo wanafanya siri.” Gazeti hili linafahamu kuwa mchezaji huyo atakabidhiwa shilingi milioni 50 kutokana na usajili huo, huku mshahara wake ikielezwa kuwa ni shilingi milioni 2.5. 

Kutokana na mkataba huo, kuna uwezekano mkubwa Ajibu ambaye ni mkazi wa Ilala akakabidhiwa nyumba ya kuishi pamoja na kutafuta usafiri mpya kama ambavyo wachezaji wengi wamekuwa wakifanya pindi wanapopata mikataba mipya au kuhamia kwenye timu mpya kwa kupewa dau nono.  Alipotafutwa Ajibu kuzungumzia hilo alisema: “Wewe umeona wapi mimi nimesaini Yanga? Sasa mimi nimesaini vipi Yanga, na kama ningekuwa nimesaini si kila mtu angeona. “Mimi ni mchezaji halali wa Simba na mkataba wangu unamalizika mwezi ujao, na hizo taarifa za kusaini mkataba wa awali Yanga sizijui.” 

Naye, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alipotafutwa kuzungumzia hilo alisema: “Suala la usajili hivi sasa tunalifanya kwa siri kubwa, hivyo nisingependa kuliweka wazi kwa kipindi hiki, ni vema tukasubiria hadi pale litakapokamilika tutaweka wazi.” Gazeti la Championi lilikuwa la kwanza kuandika juu ya usajili wa Yanga na Ajibu, Jumatatu iliyopita ambapo lilieleza juu ya mazungumzo baina ya pande hizo mbili kufika katika hatua nzuri.

No comments

Powered by Blogger.