ad

ad

Young Dee: Rapa Anayeishi Bongo kwa Bahati Mbaya

Rapa wa Bongo, David Genz ‘Young Dee’ ama ‘Paka Rapa’.
KUNA kipindi katika maisha kuna kuteleza, unaanguka kisha unainuka na kujifuta. David Genz ‘Young Dee’ ama ‘Paka Rapa’ ni mmoja kati ya wasanii waliopitia katika njia hizo.
Aliwika vilivyo na ngoma kama Kijukuu, Tunapeta na nyingine kibao lakini akapotea ghafla na alipoibuka alikiri kuwa alidumbukia katika dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya kwa zaidi ya mwaka.
Baada ya hayo, alianza tena harakati za muziki kwa kutoa ngoma kali kama Hands Up, Young Dady, Furahana sasa ameibuka na ngoma ambayo ni gumzo mtaani ya Bongo Bahati Mbaya.



Showbiz ilikutana na Young Dee ambapo alifungukia juu ya ngoma hiyo na katika makala haya anafunguka zaidi. Showbiz: Idea ya Bongo Bahati Mbaya ilikujaje? Young Dee: Ilikuja siku moja hivi nikiwa na prodyuza wangu, T Touch maana mara nyingi huwa tunakaa tunaongea. Sasa katika
kukaa tunazungumza akaniambia hivi unajua Dee wewe ni kama Bongo bahati mbaya hivi. Nikamwambia kivipi? Akasema mambo yako ni kama Bongo bahati mbaya.


 

Kuna siku tena akawa anagonga ‘beats’ akaniambia tugonge idea yoyote au tugonge Bongo bahati mbaya, nikamwambia sawa basi akigonga nikawa naimba Bongo bahati mbaya hadi ikatokea ngoma hiyo. Showbiz: Kwa muda mrefu unafanya muziki ndani ya nchi, kimataifa vipi? Young Dee: Kwa sasa hivi ni kusimama vizuri nyumbani kwanza kwani ukikubalika sana nyumbani inakuwa rahisi kutanuka kimataifa.
 

Showbiz: Baada ya kuachana na MDB nani anasimamia kazi zako za muziki kwa sasa? Young Dee: Nipo na menejimenti inayoitwa King Cash ambayo ipoMarekani na tawi lakemojawapo ni TouchesSound ambapo Touch ameniunganisha nayo na Bongo Bahati Mbaya ndiyo projekti ya kwanza kuifanya nao. Showbiz: Kwenye Video ya Bongo Bahati Mbaya anaonekana demu wako wa zamani, Amber Lulu, vipi umerudiana naye? Young Dee: Kwenye video ameonekana tu kama mmoja wa mamodo, ‘nothing personal’, hakuna kinachoendelea kati yetu, ni mshikaji tu aliyeamua kutoa shavu. Showbiz: Una mpango wowote wa kufanya ngoma na Amber Lulu maana kwa sasa naye anaimba? Young Dee: Hilo kwa sasa siwezi kuliongelea.
 

Showbiz: Vipi una mipango yoyote ya kutoa albamu? Young Dee: Mipango ipo lakini ni baada ya mwaka huu yaani mwakani mwanzoni tutaanza kutangaza michakato pia kolabo za kimataifa tutatangaza soon. Showbiz: Unaweza kutuambia siri ya muziki unaofanya? Young Dee: Siri kubwa naupenda muziki
ninaofanya. Nashirikiana na watu wanaopenda kitu ninachokifanya kama vile kina T- Touch wanaonisaidia kuongezea idea kwenye ngoma zangu na pia kutumia muda mwingi katika kufanya muziki kuliko kitu chochote.
Showbiz: Mbali na Bongo Bahati Mbaya, kuna projekti yoyote kubwa inakuja? Young Dee: Bongo Bahati Mbaya ni kama mwanzo, mashabiki wategemee projekti.

No comments

Powered by Blogger.