Siri 5 za Wema Akiwa Chadema, Kisa Umri Wake
HAKIKA kila jambo lina wenyeji wake katika utekelezaji au namna ya kulihimili kiasi cha kulifanya liendelee kuwa na nafasi sawa na maisha ya zamani. Sentensi hiyo inakuja kufuatia mabadiliko ya maisha ya sasa ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu. Staa huyo wa sinema za Kibongo kwa sasa ameamua kuingia katika maisha ya siasa kwa jumla.
Kwa mujibu wa Wema, zamani alikuwa anabipu lakini baada ya kubadili upepo na kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema) amejikuta ‘akifi chwa’ na kushindwa kuwika hivyo kuhisiwa kuwa ufalme wake unataka kupotea kutokana na staili ya maisha ya upande huo ambayo hayataki mbwembwe nyingi.
Ijumaa limefuatilia nyendo za Wema tangu siku ya kwanza alipotangaza mabadiliko yake ya maisha ya kisiasa na kuhamia rasmi Chadema ambapo limebaini kuwa kwa kiasi fulani baadhi ya ndugu na mashabiki wake wamekosa ladha yake ile ya zamani.
Wamekosa ile ladha yake ya kujichanganya kila kona na kusababisha matukio yaliyokuwa yakimfanya kutokaukiwa na vituko na vijimambo, jambo ambalo kwa sasa ni nadra sana kujitokeza. Akizungumzia na Ijumaa juu ya kufi chwa kwake, Wema anasema kwamba, siku zote unapoamua kuanza maisha mengine lazima ukubali kubadilika kwa kila jambo hivyo kwa kipindi hiki ambacho ameamua kuanza maisha mapya ya siasa, ili aweze kufi kia malengo na dhamira yake, hana budi kuchagua namna nyingine ya maisha japokuwa kuna wale ambao hawatakubaliana naye wala kuridhika na maisha aliyoyachagua kwani wapo ambapo staili yake hiyo itawagharimu.
Wema anasema kuwa, anajitahidi kuendelea kumfanya mtu ampendaye asione mabadiliko ya maisha yake, lakini pia lazima kila mmoja atambue kuwa siku na umri havisubiri. Hivyo ni lazima aanze mapema kuchagua vitu vya msingi vya kujihusisha navyo.
KUWEKEZA KWENYE SIASA
Wema anasema: “Kweli kuna watu wengi wanasema nimepotea japo sijajua wa
namaaninisha nimepotea wapi, maana nilichoamua kukifanya kwa sasa ni kuangalia mambo ya muhimu na hasa kwenye siasa ambayo ndiyo sehemu niliyoichagua kuwekeza asilimia kubwa ya maisha yangu.
KUACHA MISELE “Najua wengi wangependa kuniona nikipiga ‘misele’ kama zamani, jambo ambalo sioni tena faida yake kwani nina malengo makubwa na uamuzi wangu, hivyo nalazimika kuchagua ishu muhimu za kufanya na mahali pa kwenda hasa kunapokuwa na kitu ambacho kinaweza kunisaidia mimi au chenye malengo na maisha yangu ambayo nayatazamia hapo baadaye. “Sina maana kwamba siwezi kujichanganya na mashabiki wangu au kwenda kwenye events (matukio) mbalimbali. Ila ieleweke kwamba Wema huyu wa sasa siyo mtu tena wa kuamua tu aende mahali bila mipangilio ya aina yoyote kama ilivyokuwa awali.
STAREHE ZISIZO NA FAIDA “Kuna muda inafi kia lazima mtu uwe na chaguo sahihi la maisha yako. Zamani nilikuwa ninakwenda kila sehemu, hivyo ninajikuta ninakwenda mahali ambapo hapaniletei faida hata kidogo. Kwa sasa nitaenda sehemu ambazo naona kabisa zitaweza kuniletea jambo la muhimu na siyo kufanya mambo kwa ajili ya kuwafurahisha akina fulani tu huku mimi sipati chochote kile. “Sitaki kufanya starehe tu bila faida ndiyo maana utaona nimea
mua kubadilika mwenyewe. Kuna mambo ambayo kwa sasa sitakiwi kuyafanya.
KUWAACHA MARAFIKI “Ili kufanikisha hilo utaona hata wale marafi ki ambao hawana maana nimeamua kuachana nao kwa kuwa kuanza maisha mapya lazima ujitolee kuachana na mambo mengi ya kipuuzi.
KUKWEPA VITISHO “Watu wangu wanatakiwa waelewe kuwa kwa sasa nafurahia sana maisha yangu tangu nimejiweka hivi. Mwanzoni nilipohamia Chadema kulikuwa na vitisho vya hapa na pale, hata watu wangu wa karibu walinitaka nifanye haya, lakini kwa sasa sina tatizo wala hakuna vitisho tena. Nimeamua kujifanyia vitu ambavyo baadaye kwa yeyote anayeshindwa kunielewa leo aje kushuhudia kwa upana zaidi mafanikio haya.”
Post a Comment