ad

ad

Upungufu wa damu kwa wajawazito ni hatari sana kwa afya zao



VIFO vya wanawake wengi wajawazito, huchangiwa kwa kiasi kikubwa na kuishiwa damu wakati wa kujifungua. Utaiti unaonesha kwamba wanawake wengi hawajui kwamba upungufu wa damu ni hatari sana kwa afya zao.

Upungufu wa damu (anaemia), hutokea pale damu inapokosa chembe nyekundu za kutoha, ambazo kazi yake huwa ni kubeba hewa ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. 

Wakati wa ujauzito, mwili wa mwanamke unatakiwa kuzalisha damu kwa wingi kwa ajili ya kusapoti ukuaji wa mtoto. Hata hivyo, ili mwili uzalishe damu kwa wingi, ambayo kimsingi huzalishwa kwenye uboho wa mifupa (bone marrows), ni lazima mjamzito ale vyakula vyenye madini ya chuma na virutubisho vingine kadhaa.

Kwa mantiki hiyo, ni lazima mjamzito azingatie ulaji wa lishe bora, hasa vyakula vyenye madini ya chuma na Vitamin B 12 ambavyo huchochea uzalishwaji wa haemoglobin na mwanamke akishindwa kufanya hivi, hujikuta akipata tatizo la upungufu wa damu. Vitamin B12 hupatikana kwa wingi kwenye nyama, maziwa, mayai na siagi kwa hiyo ni muhimu mjamzito akala vyakula hivyo kwa wingi.

Dalili za awali za Anaemia, huwa ni mama mjamzito kuchoka sana na mwili kuwa dhaifu. Dalili nyingine ni ngozi kupauka, kusikia kizunguzungu, kushindwa kupumua vizuri, mapigo ya moyo kwenda mbio na kushindwa kutuliza akili.


 Hata hivyo, Anaemia inapokuwa kwenye hatua za mwanzo, mjamzito anaweza asihisi dalili zozote kwa hiyo ni muhimu kwa wajawazito kuwa na utaratibu wa kupima damu mara kwa mara.

Endapo mjamzito atashindwa kupatiwa matibabu mapema, anaweza kuzaa mtoto njiti, au mwenye uzito mdogo, anaweza kujifungua mtoto mwenye anemia, anaweza kupoteza maisha endapo atatokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.

No comments

Powered by Blogger.