ad

ad

Sababu Tatu Ngoma Ya Darasa Kubuma



UNAPOZUNGUMZIA ngoma kali zilizowahi kufanya vizuri katika historia ya Muziki wa Kizazi Kipya nchini hutoacha kuitaja Ngoma ya Muziki ya Darasa. Kabla ya kufanya Ngoma ya Muziki, Darasa alikuwa na ngoma kibao kama Sikati Tamaa, Siyo Mbaya, Weka Ngoma, Too Much na Utanipenda ambazo zilisumbua kwa kiasi chake.

Lakini gumzo kwa sasa ni juu ya ujio wake huu mpya wa Ngoma ya Hasara Roho.
Mash-abiki wengi wali-kuwa na shauku kutaka kujua ujazo wa ngoma yake hiyo kama itaweza kupiku levo za Muziki lakini imekuwa ndivyo sivyo.

Mapokeo yamekuwa kidogo ‘imebuma’, Showbizimemtafuta Darassa na kufunguka sababu tatu zilizofanya ngoma hiyo kupata mapokezi Darasa anasema, Ngoma ya Hasara Roho, maudhui na
maneno yake mengi ni ya mafumbo na hayako wazi kama ilivyokuwa kwa Ngoma ya Muziki hivyo kufanya ngoma yake kuwavutia mashabiki wachache.

“Maneno na maudhui ya kwenye ngoma yangu mpya hayako wazi, hadi usikilize vizuri ndiyo unaelewa namaanisha nini, hiyo ni sababu kuu ndiyo maana unaona watu hawajaipokea ngoma hiyo kwa mikono miwili.”

Sababu ya pili anayoitaja Darassa ni kuwa, watu wengi walipagawa na midundo ya kwenye Ngoma ya Muziki na kutaka aje na ladha ileile bilakujali muziki lazima ubadilike kila wakatiili kupata ladha mpya tofauti.

“Watu walinitabiria, wakadhani nitakuja na midundo ileile, maisha ya muziki hayawezi kuwa hivyo lazima wakati mwingine tubadilike.

Tunapobadilika ndipo changamoto kama hizi zinapojitokeza, hata hivyo napata cha kujifunza kwenye hilo.”
Sababu ya tatu na mwisho ni ngoma yake ya Hasara Roho kutopata nafasi ya kutosha kwenye vyombo vya habari kama ilivyokuwa kwa Ngoma ya Muziki.

No comments

Powered by Blogger.