MMILIKI WA SHULE YA LUCK VICENT APANDISHWA KIZIMBANI
ARUSHA: Mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent Nursery and Primary ya Arusha ambayo Mei 6, mwaka huu ilipata janga la ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, Innocent Moshi na makamu mkuu wa shule hiyo, Longino Vicent Nkana, jana wamefikishwa mahakamani na kusomewa makosa matano.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Rose Sule aliiambia mahakama hiyo kwamba, mnamo Mei 6, mwaka huu, mmiliki huyo aliruhusu dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji huku likiwa halina bima ambapo pia alishindwa kuingia mkataba na mwajiriwa huyo (dereva). Makosa mengine ni pamoja na kuzidisha abiria 13 kwenye gari hilo na kaimu mkuu wa shule kuratibu safari pamoja na kuruhusu gari kuzidisha abiria. Hata hivyo, watuhumiwa wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili na bondi ya shilingi milioni 15 kila mmoja huku washitakiwa wakizuiwa kuondoka ndani ya Mkoa wa Arusha ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria.
Hakimu wa mahakama hiyo aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Desdery Kamugisha aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 8, mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika. Wakati huohuo, majeruhi watatu wa ajali hiyo waliolazwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, wanatarajiwa kusindikizwa kuagwa kesho kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ataungana na watu wote watakaojumuika kuwaaga. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alisema kuwa, tayari ndege aina ya DC 8 imepatikana ambayo itawasafirisha watoto hao kwenda kutibiwa nchini Marekani hadi pale watakapopona.
“Ndege hiyo inatarajiwa kutumika kama ‘air ambulance’ itawasili kesho (leo) katika Uwanja wa Ndege wa Kia na hafla ya kuwaaga itafanyika Jumapili ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. “Ndege hiyo aina ya DC 8 inatokea Charlotte NC (Marekani), tayari kwa kuwachukua watoto wetu kwenda kutibiwa zaidi katika Hospitali ya Mercy, Sioux City IA,” alisema Nyalandu.

Post a Comment