ad

ad

Nikki wa Pili: Huwenda Wasafi.com ya Diamond isitusaidie

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Weusi, Nikki Wa Pili amefunguka kuzungumzia changamoto zilizopo katika platform mbalimbli za kuuza muziki nchini.



Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakulevya’, amedai Watanzania hawapendi kununua muziki huku akidai bado mambo ni magumu licha ya kunzishwa kwa platform mbalimbali za kuuza nyimbo za wasanii.

“Watanzania hawapendi kununuwa muziki, platform kama Wasafi.Com haita leta tija, kama bado unataka kupata wimbo bure kwenye ma groups ya whatsaap,” alitweet Nikki wa Pili.
Kabla ya Diamond kuanzisha kampuni ya Wasafi.Com, Mkito ndiyo kampuni pekee ya Tanzania ambayo ilikuwa ikiuza nyimbo za wasanii.

No comments

Powered by Blogger.