Nay Wa Mitego Amjibu Waziri Mwakyembe Kuhusu Kutoimba Siasa
Rapa
Nay wa Mitego amefunguka na kumtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake
aliyotoa kuwa wasanii wasijihusishe na masuala ya siasa.
Nay
wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa
Radio, amesema kuwa yeye anaamini muziki ni siasa na siasa ni muziki
hivyo ni ngumu kutofautisha vitu hivyo viwili, hivyo amemuomba Waziri
mwenye dhamana kutoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo na kudai yeye hajawahi
kuimba wimbo wa siasa bali anaimba mambo yaliyopo kwenye jamii.
"Nachoamini
mimi muziki ni siasa na siasa ni kama muziki, siasa ni maisha ya watu
ambayo wanaishi kila siku na muziki pia ni maisha ya watu ambayo
wanaishi kila siku kwa hiyo anahitaji kutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya
hili. Siasa ni maisha ya watu na muziki ni maisha ya watu, mimi binafsi
naamini sijawahi kuimba wimbo wa siasa hata siku moja bali ninaimba
maisha ya watu ambayo yanaendelea kila siku na ndiyo maana wengi
wanathubutu kusimama upande wangu endapo linatokea tatizo lolote" alisema Nay wa Mitego.
Mbali na hilo Nay aliendelea kusisitiza kuwa kuna haja Waziri kutoa ufafanuzi wa jambo hilo
"Mh.
Waziri anatakiwa kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili ili watu wajue kipi
hawatakiwi kuimba na kipi wanatakiwa kuimba sababu siasa ni maisha ya
watu ya kila siku na muziki wa Hip hop ni maisha ya watu ya kila siku,
kwangu mimi muziki wangu hauwezi kubadilika zaidi nitazidi kuongeza vitu
ili nisiwaudhi watu na nizidi kuongeza idadi ya mashabiki" alisisitiza Nay wa Mitego
Post a Comment