Mbaraka Amkana Aveva, Adai Hana Mkataba Simba
Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph
BAADA ya juzi Jumatano, Rais wa Simba, Evans Aveva kutangaza klabu hiyo ina mkataba na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbaraka Yusuph anayeitumikia Kagera Sugar ya Kagera, straika huyo ameibuka na kumkana kiongozi huyo kwa kuweka wazi kuwa hana mkataba na timu hiyo. Aveva aliweka bayana kuwa wana mkataba na straika huyo na waliidhinishiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa aichezee timu hiyo kwa msimu huu, lakini wanashangazwa na uwepo wake ndani ya kikosi cha Kagera Sugar, kilichopo mikononi mwa Kocha Mecky Maxime. Rais wa Simba, Evans Aveva akionyesha kitambulisho cha usajili cha Mbaraka Yusuph.
Mbaraka, mwenye mabao 11 kwenye ligi, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, Simba wasijisumbue kumfuatilia kwa kuwa yeye hana mkataba na timu hiyo ambayo inaongoza ligi kwa sasa. “Wao wenyewe viongozi wa Simba wanatambua kwamba mimi siyo mchezaji wao kwa sababu nilishamalizana nao tangu msimu uliopita na nacheza Kagera Sugar nikiwa mchezaji halali kabisa kwa ajili ya timu hiyo. “Kama wao Simba wana uthibitisho kwamba nina mkataba nao basi waweke wazi mkataba wao na mimi nitawaonyesha mkataba wangu ambao unanionyesha kwamba nipo huru kwa ajili ya kuitumikia timu yangu ya sasa,” alisema Mbaraka. Alipoulizwa kuhusu kadi ya usajili ambayo Aveva aliionyesha kwa waandishi wa habari juzi, ikiwa na jina la Mbaraka Yusuph akitambulishwa kama mchezaji wa Simba, Mbaraka alisema: “Kadi ile ni ya U-20, wakati huo nilikuwa naichezea Simba kabla ya kupelekwa kwa mkopo Kagera, muda wake ulishaisha, nikasaini mkataba Kagera Sugar ambao nao unaisha mwishoni mwa msimu.”
CHANZO: CHAMPIONI

Post a Comment