ad

ad

Maswali ya Tundu Lissu kwa Mpelelezi, Kesi ya Wakurugenzi JamiiMedia…

 
Tulipokea barua kutoka JamiiForums, ilitoa maelezo marefu lakini haikuwa na majibu chanya tuliyoyaomba. Walihoji mamlaka ya polisi kutaka taarifa hizo na kusema wana haki ya usiri wa taarifa za wateja wao(Hakimu anaoneshwa barua).

REJEA YA MADA TAJWA: USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar =====
Shahidi anasema anaikumbuka barua ile aliiona kwa macho yake na anaiomba aitoe mahakamani kama kielelezo. Shahidi anaambiwa aisome barue.
Wakili anamuuliza shahidi ana maoni gani kuhusu barua kutoka Jamii Forums, Shahidi anasema yeye hajaona taarifa yoyote ya faragha katika zile walizoomba.
Anaendelea kuwa tarehe 01/04/2016 waliandika barua nyingine kukumbushia taarifa hizo na walinukuu kifungu cha 10 subsection 2-8 ya Crime Procedure Act.
Kifungu hicho kinawapa mamlaka polisi kupata taarifa kutoka ofisi yoyote kama taarifa iko relevant na suala linalofanyiwa upelelezi. Baada ya barua hiyo JamiiForums hawakujibu tena, hivyo tukaona kuwa wanadhoofisha upelelezi wetu tukaamua tuwakamate wakurugenzi.
Anaulizwa lini walichukua uamuzi wa kuwakamata? Anajibu baada ya kuwa wamefungua shauri.
Una lingine la kuongezea? “Mheshimiwa sina”
===========
Baada ya hapo akaingia wakili Tundu Lissu na kusema ana maswali mengi.
Tundu Lissu Anasema aeleze kisomo chake mpaka amekuwa SSP wa polisi.
Shaidi anasema: 2001 May aligraduate CCP kama constable wa polisi, 2002 feb-july 2003 alipata Assistant inspector.
2006 December, ass inspector to full inspector wa polisi.
2009 Feb-July alienda mafunzo ya uofsa na kuwa ASP wa polisi.
2014 akiwa katika ulinzi wa amani Sudan alipanda from ASP to SSP.
Mwaka jana ndiyo akawa SSP.
Tundu Lissu: Kwa maelezo yako ni sawa nikisema wewe ni afisa wa polisi mwenye uzoefu wa upelezi wa makosa ya jinai? Jibu: Ndio
Tundu Lissu: Ni sahihi kuwa una uzoefu wa upelelezi ndani na nje ya nchi? Jibu; Ndio
Tundu Lissu: Kwa mujibu wa maelezo yako taarifa ya Usama Mohammed ndio ilipelekea mfungue jalada? Jibu: Ndio
Tundu Lissu: Na ndio zilipelekea muandike barua kwa Jamii Forums 23 February 2016? Jibu: Kweli
Tundu Lissu: Naomba umueleze hakimu kama hiyo barua iko mahakamani. Jibu: Haipo.
Tundu Lissu: Sasa shahidi mimi ninayo hiyo barua (anampa shahidi na kumwambia aiangalie). Tundu Lissu: “Angalia hiyo barua SSP Kingai”
Tundu Lissu Anamwambia amwambie mheshimiwa hakimu kama ile barua imeandikwa kwa Maxence Melo. Jibu: Haijataja jina la mtu
Tundu Lissu: Kwahiyo jina la Max Melo Mubyazi halipo? Jibu: Halipo
Tundu Lissu: Je! Imeelekezwa kwa Mike William? Jibu: Haijataja jina
Tundu Lissu: Sasa naomba useme kama kwenye hiyo barua mmesema kuwa mmepata taarifa toka kwa Usama Mohammed? Jibu: Hatujaandika na hatukuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Tundu Lissu
: JamiiForums ni kampuni??
Jibu: Ni kampuni
Tundu Lissu: Kama ni kampuni inatakiwa aiandikishwe Brela, hati ya kuandikishwa Brela iko wapi? Jibu: Mheshimiwa mimi natoa ushahidi kama mtoa maelekezo, walioandika hizo barua watakuja na kueleza.
Tundu Lissu: Nauliza iko wapi? Yaani iko mahakamani sasa? Jibu: Ndio
Tundu Lissu: Kama kampuni inatakiwa iwe na Memorandum of Association, iko wapi? Jibu: Sifahamu.
Tundu Lissu: Taarifa za ukwepaji kodi za Fahrer mlizi-print?? Jibu: Sijui kama ziliprintiwa
Tundu Lissu: Kwa hiyo ziko wapi? Wewe si ndio kiongozi wa upelelezi Jibu: Hazipo mahakamani kwa sasa.
Tundu Lissu: Unataka hakimu azifate shimoni? Jibu: Mimi ni shahidi mmoja kati ya wengi wengine watakuja nazo.
Shahidi amesoma barua toka kwa wanasheria wa JF. Kipande kimoja kinasema “mteja wetu yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa mujibu wa sheria”
Tundu Lissu anamuuliza sasa ” ulisema kuwa katika barua hiyo JF ilijibu kuwa ina wajibu wa kulinda faragha za wateja wao. Kwa ufahamu wako kuna haki ya kila mtu kulindiwa faragha ya mawasiliano yake au hakuna?” Jibu: Inategemea
Tundu Lissu: Haki ipo au haipo?? Jibu: Kwa private person sifahamu…
Tundu Lissu: Kwa ufahamu wako kuna haki ya kulindiwa faragha ya mawasiliano kwa kila mtu including private persons? Jibu: Sifahamu
Tundu Lissu: Barua ile ya kutoka kwa wanasheria wa JF inasema ” mteja wetu anaomba ufafanuzi wa sheria itumikayo kuomba taarifa za mteja” kwa uelewa wako mtu anayeomba ufafanuzi amekataa kutoa taarifa au hajakataa? Jibu: Kwa maelezo hayo amekataa.
Tundu Lissu: Mtu anayeandika kuwa ” mteja wetu angependa kujua kipi cha sheria kinatumika kuomba taarifa za mteja ukiacha kifungu namba 32 cha Cyber Crime Act” Mtu aliyeuliza ni kifungu kipi cha sheria kinatumika amekataa kutoa taarifa au hajakataa? Jibu: Kwa maelezo hayo ya sasa hajakataa.
Tundu Lissu: Umesema baada ya kupokea barua ya kutoka kwa wanasheria wa Jamii Forums mliandika nyingine 1/4/2016… Je iko mahakamani? Jibu: Sina uhakika nadhani ipo mahakamani.
Hakimu: Mimi sina.
Tundu Lissu: Mimi ninayo.
Hakimu: Haiwezi kutumika wakati mimi sina haijafika mahakamani.
Tundu Lissu: Inaweza tumika sababu ameitaja.
Tundu Lissu: Mweleze hakimu kama barua imewataja watuhumiwa. Jibu: Haijawataja.
Tundu Lissu: Kwenye ushahidi wako wa msingi umesema kuwa barua hii haikujibiwa si ndio? Jibu: Sijui kama haikujibiwa.
Tundu Lissu: Wewe ni msimamizi gani wa upelelezi usiyejua taarifa muhimu. Jibu: Sikupata taarifa kama imejibiwa
Tundu Lissu akatoa barua toka kwa Victory attorneys iliyojibu barua ile ya 01/04/2016.
Tundu Lissu: Shahidi tafadhali ieleze mahakama kama barua hiyo haina mhuri wa kupokelewa na ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar Jibu: Sina uhakika na Mhuri huu na wala Mhuri sina uhakika nao.
Tundu Lissu: Naomba uulinganishe mhuri huo na ule wa kwenye exhibit PI (barua ya majibu ya mwanzo) Jibu: Mimi sio expert wa hayo mambo siwezi kulinganisha.
Tundu Lissu: Tusomee hiyo document imeandikwa kupokewa lini Jibu: Kwa mujibu wa document hiyo inaonesha ilipokewa 06/05/2016
Wakili wa serikali anaobject hapo Kuwa, shahidi hawezi kuendelea kuhojiwa kwa document asiyokuwa na uhakika nayo.
Tundu Lissu: Naomba barua hii iwe admitted in evidence for purposes of impeaching….(itumike kama kielelezo)
Upande wa serikali: Shahidi aliyesimama mahakamani ameletwa na Jamhuri, kumu-impeach shahidi ni kwa yule aliyemwita mahakamani….
Lissu hawezi kumu-impeach shahidi aliyeletwa na Jamhuri. Purpose of cross examination ni kucheck credibility ya shahidi…hawatakiwi kumuimpeach…wasubiri muda wa defence kutumia hizo documents…shahidi hawajamleta wao. Au wanipe kifungu wanachotumia kutaka kumuimpeach shahidi.
Tundu Lissu anatoa kifungu… Hakimu anapelekewa akisome 164 (1).
Baada ya kusoma hicho kifungu, Hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 4 asubuhi kesi hiyo itaendelea.

No comments

Powered by Blogger.