ad

ad

MANCHESTER UNITED MABINGWA EUROPA LEAGUE, WAREJEA UEFA CHAMPIONS LEAGUE


Kocha Jose Mourinho ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni mtu wa mataji baada ya kuiongoza Manchester United kutwaa ubingwa wa Europa League.

Man United imeifunga Ajax mabao 2-0 na kutwaa ubingwa huo ambao umewawezesha Man United kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mujibu wa kanuni za Europa League ni kuwa bingwa anapata nafasi ya kushiriki katika Ligi ya Mabingwa.

Ushindi huo umekuwa furaha kubwa kwa wadau wote wa United kutokana timu hiyo kupitia kipindi kigumu cha kuwa na majeruhi wengi kiasi cha kulazimika United kushika nafasi ya sita katika msimamo wa Premier League msimu huu uliomalizika wa 2016/17.

























No comments

Powered by Blogger.