ad

ad

IGP Simon Sirro: Kazi yangu ni kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amefunguka na kusema uhalifu haulipi huku akiwaahidi Watanzania kuwa kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha jamii inaishi kwa amani bila hofu ya wahalifu.

IGP Sirro amesema katika utawala wake atahakikisha vitendo vya uhalifu vinapungua kama sio kuisha kabisa kwenye jamii huku akihimiza wananchi kuonesha ushirikiano ili kuweza kutimiza azma yake.
“Kazi yangu ni kuhakikisha uhalifu unapungua kwa kiasi kikubwa ili Watanzania waweze kuishi kwa amani, lakini uhaliofu huo utapungua nikipata ushirikiano na jamii, kwasababu hawa wahalifu wanaishi katika jamii kwahiyo ombi langu ili tuweze kuishi kwa ulinzi na usalama na utulivu ni vizuri wakatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, kwasababu wahalifu ni wengi na sisi ni wachache,” amesema IGP Sirro huku akiwaonya wahalifu
“Lakini niwape onyo wahalifu siku zote uhalifu haulipi, kunga’nga’nia uhalifu mwisho wa siku utaacha familia yako ni afadhali urfanye kazi ya halali ambayo itasaidia kulea familia yako lakini ukijiingiza kwenye mambo ya ujanja ujanja haitakusaidia kitu mwisho wa siku utaacha familia yako.”

Na Emmy Mwaipopo

No comments

Powered by Blogger.