ad

ad

HANS POPPE ABADILI MAAMUZI, AREJEA KWENYE NAFASI YAKE SIMBA

Muda mfupi baada ya taarifa kutoka ndani ya Simba kuwa Zacharia Hans Poppe amejiondoa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba, sasa kuna mabadiliko na habari ni kuwa amerejea klabuni hapo aktika nafasi yake.


Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa baadhi ya viongozi ‘wazito’ wa Simba walikutana na Hans Poppe, jana usiku na kuzungumza naye hadi usiku wa manane kabla ya kumfanya abadilia uamuzi wake huo.

Mtoa taarifa kutoka ndani ya Simba amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kikao kilichodumu muda mrefu kwa kuwa kuondoka kwa Hans Poppe katika nafasi yake ni jambo kubwa na ambalo lingekuwa pigo kwa Klabu ya Simba kutokana na mchango wake klabuni hapo.

Hans Poppe amekuwa akisaidia Simba katika masuala kadhaa hasa ya usajili ambapo imefahamia amekuwa akifikia hatu ya kutoa fedha zake za mfukoni kwa kuikopesha klabu kama ambavyo wadau wengine kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kifedha wamekuwa wakifanya.

Awali, Hans Poppe kabla ya kutokea hicho kilichotokea inaelezwa kuwa Hans Poppe alifikia uamuzi huo kutokana na kuona kuna baadhi ya mambo hayaendi sawa, huku suala la mkataba wa Simba na Kampuni ya Sportpesa ukitajwa kuhusika.

No comments

Powered by Blogger.