Taarifa ya Wizara ya Habari kuhusu kutoweka kwa Roma Mkatoliki
Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo imesema imepokea
kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina
la kisanii “Roma Mkatoliki” tangu tarehe 5 Aprili 2017.
Katika
taarifa yake iliyotolewa jana jioni na kusainiwa na Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa wizara Zawadi Msalla, alisema kuwa
wizara hiyo kwa dhamana yake katika tasnia ya sanaa, imefuatilia kwa
karibu suala hilo kwa kuwa lina muelekeo wa jinai na kwamba hashikiliwi
katika kituo chochote cha polisi.
"Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi".Alisema Zawadi.
Alisema
kutokana na hali hiyo, wizara imewaomba wadau mbalimbali na wananchi
kwa ujumla kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote
zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.
Post a Comment