Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mrembo wazua maswali
Picha ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mrembo zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zimezua maswali kwa baadhi ya mashabiki zake kwamba inawezekana ndiye mrithi wa mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni mzazi mwenzake, Faiza Ally.
Mashabiki mbalimbali walionesha kuifurahia picha hiyo na kusema kapo yao inaendana kama ndiye mchumba wake huku wakitaka kujua ukweli kama ndiye mchumba wake lakini yakawa ni maswali yasiyo na majibu kwani hajawahi kuyajibu.
“Naona Sugu ameamua kumwanika mchumba wake maana asingeweza kuposti picha kama hii wakiwa katika pozi kama siyo mtu wake, kapo yao ni nzuri sana natamani wangefunga ndoa hata leo,” alisema shabiki mmoja. Ili kuujua ukweli Risasi Jumamosi lilimtafuta Sugu kwa njia ya simu na kugoma kuzungumzia ambapo mahojiano yalikuwa hivi.
Risasi: Mheshimiwa nimekupigia simu hupokei nina shida ya kuzungumza nawe, mimi ni mwandishi wa habari. Sugu: Niko kikaoni, sorry ni mwandishi wa wapi na ulitaka kuzungumza kuhusu nini? Risasi: Mwandishi wa Global Publishers, kuna picha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii ukiwa kwenye pozi na mrembo ambaye inasemekana ni mchumba wako, mashabiki wanapenda kuujua ukweli na mipango ya ndoa ikoje? Sugu: Kimya. Risasi: Mheshimiwa mbona kimya? Sugu: Kimya lakini meseji anazisoma. Mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni hakuwa amejibu chochote licha ya kutumiwa pia picha hiyo kwa njia ya WhatsApp
Post a Comment