RONALDO APIGA HAT TRICK MADRID IKIINYOOSHA BAYERN 4-2 NA KUTINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA
Achana
na zile habari za hovyo za mambo ya rufaa inayoendelea Bongo, Ulaya ni
soka tu na Cristiano Ronaldo ameendelea kuthihirisha yeye ni hatareee
baada ya kupiga hat trick wakati Real Madrid ikiitwanga Bayern Munich
kwa mabao 4-2 na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Madrid
inakwenda nusu fainali kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya ushindi wa mabao
2-1 mjini Munich na yote mawili ya Madrid yalifungwa na Ronaldo.
Kwa
mabao hayo, maana yake Ronaldo amefikisha mabao 103 aliyofunga katika
michuano ya Ulaya ngazi ya klabu. Leo aliingia uwanjani akiwa na mabao
100 baada ya kufunga mawili mjini Munich.
Bayern
walianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa mkwaju wa penalti
kupitia Robetro Lewandowski, Madrid wakasawazisha dakika ya 76 akifunga
Ronaldo kabla ya beki Sergio Ramos kujifunga dakika mbili baadaye.
Kipigo
cha 2-1 kwa Madrid kilisababisha kuongezwa kwa dakika 30 na ndipo
Madrid ilipoanza kuporomosha mvua ya mabao, Ronaldo akifunga dakika ya
106 kwa pasi ya Ramos na Marcelo akawachambua mabeki wanne kabla ya
kumpa pasi safi Ronaldo aliyefunga bao la nne dakika ya 110.
Marco
Asensio ndiye aliyefunga bao la nne katika dakika ya 112 na kumaliza
kazi dhidi ya Bayern ambao walicheza pungufu kuanzia dakika ya 84 baada
ya Arturo Vidal kupigwa “umeme”.
Real Madrid starting XI: Navas; Carvajal, Ramos, Nacho, Marcelo; Casemiro, Kroos, Modric; Isco, Benzema, Ronaldo
Substitutes: Kiko Casilla, James, Kovacic, Lucas Vazquez, Asensio, Morata, Danilo
Bayern Munich starting XI: Neuer, Lahm, Boateng, Hummels, Alaba, Robben, Alonso, Vidal, Thiago, Ribery, Lewandowski
Substitutes: Ulreich, Bernat, Kimmich, Costa, Rafinha, Coman, Muller
Post a Comment