Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo
tarehe 23 Aprili 2017 imekamilisha mapitio ya maamuzi ya Kamati ya
Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Masaa 72). Baaada ya Mapitio
hayo Kamati imeamua yafuatayo: I. Kamati imebatilisha maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji wa Usimamizi wa Ligi kwa sababu zifuatazo:
1.
Malalamiko ya Klabu ya Simba kutowasilishwa kwa wakati kwa mujibu wa
kanuni 20(1) ya Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2016 inayotaka malalamiko
yoyote yanayohusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi Bodi ya Ligi
Kuu sio zaidi ya masaa 72 baada ya mchezo kumalizika.
2.
Malalamiko hayo hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni 20(4) kinachosema
ada ya malalamiko ni Shs. 300,000/= (Shilingi laki tatu). Malalamiko
yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada au baada ya muda uliowekwa
hayatasikilizwa.
3. Kikao cha Kamati ya Usimamizi na
Uendeshaji wa ligi kilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha wajumbe
waalikwa ambao sio sehemu ya kamati hiyo.
Hivyo,
matokeo ya mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Simba Sports Club yanabakia
kama yalivyokuwa awali (2-1).
Vilevile Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi
za Wachezaji imemwagiza Katibu Mkuu wa TFF kuwapeleka katika Kamati za
kinidhamu na Maadili baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Ligi kwa
kutowajibika katika nafasi zao na kuipotosha Kamati ya Usimamizi na
Uendeshaji wa Ligi. IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).
Post a Comment