KADI TATU ZA NJANO WANAZOZIKATIA RUFAA SIMBA HIZI HAPA
Simba imekata rufaa ikitaka kupewa pointi tatu baada ya kupoteza mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyoitwanga kwa mabao 2-1.
Simba inadai mchezaji Mohamed Fakhi aliyewahi kuwa mchezaji wao, alicheza mechi dhidi yao akiwa na kadi tatu za njano.
![]() |
FAKHI |
Kadi zinazodaiwa na Simba ni hizi
zifuatazo na Fakhi alipata kwa nyakati tofauti ingawa Kocha wa Kagera
Sugar, Mecky Maxime amesisitiza yeye ni makini na anajua Fakhi ana kadi
mbili tu.
Desemba 17, 2016
1. Katika mchezo namba 122 dhidi ya Mbeya City uliopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Januari 18, 2017
2. Katika mchezo namba 165 Uwanja wa Kaitaba, walikipiga dhidi ya African Lyon ya Dar es salaam.
Machi 4, 2017
3. Na katika mchezo namba 190 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Walicheza na Majimaji ya Songea.
Mechi hizi ndizo ambazo zimewafanya
Simba SC kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa kumchezesha mlinzi wao Mohamedi
Fakhi katika mechi ya April 2, 2017 Kaitaba ambapo Simba alifungwa goli
2-1.
Kama madai haya yatakuwa kweli kwa ushahidi wa mechi hizo tatu , ina maana Simba watapewa alama tatu za mchezo huo waliopoteza.
Post a Comment